Mavazi ya Mwanaspoti Muislamu yazua zogo

Image caption Mavazi ya Mwanaspoti Muislamu yazua zogo

Mwanasarakasi Muislamu wa kike aliyeshinda nishani mbili za dhahabu katika michezo ya kunyosha viungo vya mwili amekashifiwa kwa kuvalia nguo zilizom'bana na kuonyesha viungo vyake vya mwili.

Licha ya kuibuka mshindi katika vitengo viwili, mwakilishi wa Malaysia, Farah Ann Abdul Hadi, 21, alikashifiwa na walimu na viongozi wa kidini kufuatia picha zake zilizoonyesha mapaja na makalio.

Image caption Mwalimu mmoja wa kidini nchini humo alisema kuwa wanawake hawapaswi kushiriki mashindano ya sarakasi.

Mwalimu mmoja wa kidini nchini humo alisema kuwa wanawake hawapaswi kushiriki mashindano ya sarakasi.

Sheikh Harussani Zakaria ''kwa kweli kuonyeshwa kwa mwili wa mwanamke kama ilivyoonekana mwili wa Farah Ann haipendezi ,ni harama''kuambatana na dini ya Kiislamu.

Image caption Bi Farah Ann Abdul Hadi alishinda jumla ya nishani 6

Bi Farah Ann Abdul Hadi alishinda jumla ya nishani 6 katika mashindano hayo kusini mwa Asia

''Ikiwa ni lazima mwanamke ashiriki mashindano ya sarakasi 'sharti ajistiri uchi wake hivyo itakuwa kheri kwa wale wanaomtizama iwe ni wanaume ama wanawake alisema sheikh Zakaria.

Image caption Farah Ann Abdul Hadi, 21, alikashifiwa na walimu na viongozi wa kidini kufuatia picha zake zilizoonesha mapaja na makalio yake

''''Ikiwa katika kandanda wanawake wanavalia suruali zinazofunika magoti yao itakuwaje wanawake waislamu wasivalie nguo kama hizo ?

Maoni yake hata hivyo yanapingwa na mwenyekiti wa shirikisho la wanawake bi Roszida Kamaruddin, ambaye anasema kuwa wanawake wasikatazwe kushiriki michezo ambayo wanatalanta.

Image caption Mwalimu mmoja wa kidini nchini humo alisema kuwa wanawake hawapaswi kushiriki mashindano ya sarakasi.

'' Ningependa wanawake wasikatazwe kushiriki mashindano haya ya sarakasi (Gymnastics) japo ningeshauri wajali mitindo tamaduni na sheria za kiislamu'' alisema Bi Roszida.

''Nawajua wanawake wengi tu ambao wanavipaji na ni washindi ila wanazingatia sheria za mavazi kwa waislamu''.

Maelfu ya mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii walimtumia jumbe za kheri njema baada ya ufanisi wake mkubwa.