Taifa Queen ya Tanzania kuelekea Namibia

Image caption Taifa Queens wakabidhiwa tiketi kuelekea Michuano ya Afrika

Timu ya taifa ya mpira wa pete ya Tanzania (Taifa Queens) imekabidhiwa tiketi tayari kwa safari ya kuelekea Windhoek, Namibia kwa ajili ya kushiriki michuano ya Afrika.

Michuano hiyo itaanza Jumapili na nchi kadhaa kama vile Kenya, Uganda zikitegemewa kushiriki.Wachezaji 16 watachaguliwa Alhamisi kwa ajili ya safari hiyo iliyodhaminiwa na benki ya wanawake, Covenant.Kikosi kizima cha Taifa Stars kinajumisha wachezaji wafuatao, ambao miongoni mwao 16 watachaguliwa.

Restituta Boniface, Veronica George (Ikulu), Penina Mayunga (JKT), Bertina Kazinja (Magereza), Nasra Suleiman, Faraja Malaki (JWTZ), Jawa Idd (Polisi Moro), Fatma Fussi (Ofisi ya Rais Utumishi), Irene Elias, Sophia Komba (Nahodha), Nahodha Msaidizi Lilian Sylidion (Ofisi Rais Ikulu), na Ndigwako William (Polisi Dar).

Wengine ni Mainda Rodgers (Mafunzo), Tatu Ally, Joyce Adeck (Utumishi), Siwa Juma (Mafunzo), Minza Nyange (JKU), Faraja Malaki (JWTZ), na Sharifa Mustapha (Uchukuzi).

Viongozi watakaoambatana na timu ni Annie Kibira, Rahma Ally Hamis kutoka Zanzibar , Hilda Mwakatobe (Chaneta), huku makocha ni Edson Chitanda (Bara), na Hafsa Abraham ( Zanzibar ).