England yaiondoa Canada :Kombe la Dunia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Timu ya wanawake ya England ilifuzu kwa mara ya kwanza katika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia baada ya kuilaza Canada 2-1

Timu ya wanawake ya England ilifuzu kwa hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia ya Mashindano hayo baada ya kuilaza Canada 2-1

Ushindi huo wa kihistoria wa England sasa umewapa fursa ya kuchuana na Japan.

''The Lionesses'' kama wanavyofahamika England walijikakamua kuhimili mashambulizi ya wenyeji hao kabla ya kiungo wao Jodie Taylor,kutumia vyema makosa ya mlinzi wa Canada Lauren Sesselmann na akaiweka Uingereza mbele kwa bao la kwanza.

Taylor ambaye alikuwa anarejea mashindanoni kwa mara ya kwanza tangu afanyiwe upasuaji wa goti wikitisa zilizotangulia alikuwa mwiba katika safu ya ulinzi ya Canada.

Haikujalisha kuwa Canada walikuwa wanafurahia mashabiki zaidi wanyumbani ,Taylor wa Uingereza aliwanyamazisha kunako dakika ya 11 ya kipindi cha pili.

Hata kabla kivumbi hakijatulia ,Mashambulizi ya England yalizaa matunda dakika 3 baadaye.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption England ilifuzu kwa hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo

Lucy Bronze alifunga bao la pili baada ya kufunga kwa kichwa mkwaju safi tu wa Freekick ulipigwa na Fara Williams.

England itajilaumu yenyewe kwani walitawal mechi hiyo hadi dakika za mwisho mwisho za kipindi hicho cha kwanza utepetevu wa safu ya ulinzi wa England ulipoitunuku Canada bao la kufutia machozi.

Kimsingi kipa wa England Karen Bardsley alifanya makosa yaliyomruhusu Christine Sinclair kufufua matumaini ya wenyeji.

Kufuatia ushindi huo sasa England watalazimika kumakinika zaidi dhidi ya Japan ambao ni wazoefu katika hatua hiyo.