Ramos kunyakuliwa na Machester United?

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Sergio Ramos

Timu ya Manchester United ya Uingereza inaamini kuwa Sergio Ramos mwenye umri wa miaka 29 anataka kuondoka Real Madrid baada ya timu hiyo kushindwa kumwongezea mkataba, ambapo mkataba wa sasa unamalizika mwaka 2017.

Manchester United imependekeza kitita cha pauni milioni 28.6 kwa Real Madrid ili kumnyakua mlinzi wake Sergio Ramos.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania ameichezea timu ya Real mara 445.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ramos alijiunga na Real akitokea timu ya Sevilla mwaka 2005.

Kocha wa Manchester United Louis van Gaal anataka kuimarisha sehemu ya ulinzi ili kuisaidia timu yake kufanya vizuri katika michuano ya ligi kuu ya England ambapo msimu uliopita alishika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo.

Ramos alijiunga na Real akitokea timu ya Sevilla mwaka 2005.

Ameichezea timu ya taifa ya Hispania mara 128 na alikuwa katika kikosi cha kwanza wakati waliposhinda kombe la Ulaya mwaka 2008, 2012 na Kombe la Dunia mwaka 2010.