Demba Ba ajiunga na Shanghai Shenhua

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Demba Ba

Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Demba Ba amejiunga na timu ya Shanghai Shenhua akitokea timu ya Besiktas ya Uturuki.

Ba mwenye umri wa miaka 30 alikua anatarajiwa kurudi katika ligi kuu ya England, lakini ameamua kuelekea mashariki ya mbali kusakata kabumbu.

Mchezaji huyu wa zamani wa vilabu vya Newcastle na Chelsea, alifunga mabao 27 katika michezo 44 aliyoicheza timu ya Besiktas, msimu uliopita.

Nyota huyu wa kikosi cha simba wa Teranga(Senegal) nyota yake ilianza kungara mwaka 2005 katika klabu ya Rouen kabla ya kuelekea Ubelgiji alikocheza kwa msimu mmoja katika timu ya Mouscron.

Baadae akatimkia Ujerumani kwa miaka 4 akiitumika klabu ya Hoffenheim msimu wa 2011 akajiunga na wagonga nyundo wa London West Ham.

Baada ya kufanya vizuri na West Ham akajiunga na Newcastle katika msimu wa 2011/12alipofunga mabao 29 katika michezo 57 kabla ya kuhamia Chelsea na kucheza michezo 51 akizifumania nyavu mara 14.