Washukiwa wa FIFA watakiwa Marekani

Haki miliki ya picha a
Image caption washukiwa wa FIFA

Marekani imewataka wakuu nchini Uswizi kuwasafirisha hadi Marekani maafisa saba wa shirikisho la kandanda Duniani FIFA waliokamatwa mwezi Mei.

Maafisa wa mahakama wa serikali ya Uswizi, wamesema kuwa polisi nchini humo watawasikiza kwanza maafisa hao wa zamani wa FIFA kuhusiana na ombi hilo la Marekani.

Na watakuwa na siku kumi na nne ili kutoa jibu.

Maafisa hao wakuu wa FIFA walitiwa mbaroni baada ya kushukiwa kupokea na kulipa mamilioni ya dola kwa njia ya ufisadi.

Miongoni wanaozuiliwa ni naibu rais wa FIFA katikati na kaskazini mwa Amerika Bwana Jeffrey Webb.