Liverpool kumsajili Benteke

Haki miliki ya picha Getty
Image caption benteke

Liverpool imekubali kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke kulingana na mtandao wa Talksport.

Liverpool imehusishwa na uhamisho wa raia huyo wa Ubelgiji katika majuma ya hivi karibuni na kulingana na Graham Beecroft mkataba unatarajiwa kuwekwa hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa kipindi cha Alan Brazil alisema:Ninavyojua ni kwamba Benteke ambaye amekuwa akiwindwa na Liverpool kwa mda sasa yuko karibu kuingia mkataba na Liverpool.

''Natarajia kwamba ataweka sahihi yake na kama si leo basi hivi karibuni.Tayari Liverpool imefanya uwezo wake na imeingia katika makubaliano''.

Mkufunzi wa Liverpool Brendan Rodgers amewasajili wachezaji watano msimu huu akiwemo James Milner,Danny Ings,Adam Bogdan,Joe Gomez na Roberto Firmino huku makubaliano ya kumsajili beki wa Southampton Nathaniel Clyne yakitarajiwa.