Calderon:Ramos angependa kujiunga na Man U

Haki miliki ya picha PA
Image caption Sergio

Beki wa Real Madrid Sergio Ramos ataihama kilabu yake ili kujiunga na Manchester United kulingana na aliyekuwa rais wa Real Madrid Ramon Calderon.

Manchester United wanamtaka beki huyo kwa kitita cha pauni milioni 28.6, ambaye wanaamini anataka kuondoka na Calderon anaamini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoka Spain anataka kuhama.

''Najua Sergio amemtaka mkurugenzi mkuu kusikiza maombi kutoka kwa klabu ya Manchester United,''alisema Calderon ambaye alihudumu kama rais wa kilabu hiyo kutoka mwaka 2006 hadi 2009.

Image caption Ramon Calderon

''Yeye angependa kwenda Manchester United pekee''.

Kumekuwa na madai kwamba Ramos anatumia uvumi huo ili kuanzisha mazungumzo ya kandarasi ilioimarika katika klabu ya Real Madrid,kilabu aliyojiunga nayo kutoka Sevilla kwa kitita cha yuro milioni 27 mwaka 2005.