Fenerbahce kumsajili Nani wa Man United

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nani

Mchezaji wa klabu ya Manchester United Nani anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa matibabu katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahce baada ya vilabu hivyo viwili kukubaliana ada ya yuro milioni 6 kwa uhamisho wa mchezaji huyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alihamia Manchester United kutoka klabu ya Sporting Lisbo ya Ureno.

Alicheza msimu uliopita katika kilabu ya Sporting Lisbon na kufanikiwa kufunga mabao 11.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Fenerbahce

Fenerbahce inasema kuwa mazungumzo ya uhamisho wa mchezaji huyo yanaendelea na kwamba Nani atakuwa mjini Istanbul ili kufanyiwa ukaguzi wa matibabu.

Nani ameshinda mataji manne ya Ligi ya Uingereza na moja la vilabu bingwa Ulaya akiichezea Manchester United.

Alitia sahihi mkataba wa miaka mitano na kilabu hiyo mwaka 2013