Mancity kutumia pauni milioni 100 msimu huu

Haki miliki ya picha
Image caption Paul Pogba

Manchester City wanatarajiwa kutumia pauni milioni 100 ili kuwasajli wachezaji wapya msimu huu baada ya vikwazo walivyowekewa kuhusu ununuzi wa wachezaji kuondolewa na UEFA.

City ilipigwa faini ya pauni milioni 49 na kulazimishwa kutoa kikosi chenye upungufu wa wachezaji 21 msimu uliopita baada ya kukiuka sheria za UEFA.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raheem Sterling

Lakini baada ya kuafikia masharti hayo ,timu hiyo sasa iko huru kuwasaka wachezaji wapya akiwemo Paul Pogba,Kevin De Bruyne na Raheem Sterling.

Ununuzi wa mchezaji wa Aston Villa Fabian Delph atakayegharimu pauni milioni 8 pia unatiliwa maanani,huku Barcelona ikiongoza harakati za kutaka kumsajili Paul Pogba.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption fabian Delph wa Aston Villa

Lakini licha ya kupewa ruhusu ya kufanya matumizi inavyotaka katika dirisha la uhamisho,City imeonywa kwamba fedha zake zitaendelea kuchunguzwa ili kuhakikisha kuwa inaafikia masharti makali yaliowekwa.