Chile ndio mabingwa wa Copa America

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chile

Chile imewashinda Argentina kupitia kwa mikwaju ya penalti na kushinda kombe kubwa zaidi kati ya nchi za Marekani ya kusini la Copa Amerika.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sanchez

Hili ndilo kombe la kwanza la kimataifa kuwahi kushindwa na Chile.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Chile

Chile ambayo ni waandalizi waliwashinda Argentina mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penalti baada ya timu zote kukosa kufunga.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachezaji wa Argentina

Ni miaka 22 tangu Argentina washinde kombe lolote kubwa kwenye mashindano ya kandanda ya kimataifa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki

Mchezaji wa Arsenal Alexis Sanchez alifunga bao la ushindi baada ya mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain kupiga nje huku mkwaju wa Ever Banega ukinyakwa na kipa Claudio Bravo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vidal

Awali Higuain alikuwa amekosa bao la wazi aliposalia na kipa baada ya dakika 90 za mchezo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Messi kwa mara nyingine ashindwa kuipatia taifa lake taji

Sanchez karibia afunge katika dakika za ziada.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Higuain akikosa penalti

Miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliojaa kuishabikia timu yao ni wachimba mgodi 33 waliokwama chini ya mgodi kwa wiki kadhaa mwaka 2010,katika kisa kilichovutia hisia nyingi duniani.