Blatter alaumu Ufaransa na Ujerumani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sepp Blatter

Rais wa shirikisho la soka Duniani, FIFA, ameishutumu Ufaransa na Ujerumani kuwa zilitumia chagizo za kisiasa, kutaka Urusi na Qatar kuchaguliwa kuwa wenyeji wa kombe la dunia, la miaka 2018 na 2022.

Akizungumza na gazeti la Ujerumani (Welt am Sonntag), Sepp Blatter, alidai kuwa rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, na mwenzake wa Ujerumani, Christian Wulff, walijaribu kuwashawishi wawakilishi wa nchi zao, kabla ya kura.

Bwana Blatter, ambaye sasa anachunguzwa na shirika la uhalifu la Marekani, FBI, kuhusu tuhuma za rushwa, amesema amechoka kubeba lawama kwa jambo ambalo halikuwa mikononi mwake .