Marekani bingwa kombe la Dunia wanawake

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji wa Marekani wanawake wakishangilia ushindi

Marekani imeibuka mshindi wa Kombe la Dunia soka wanawake kwa kuichabanga Japan kwa bao 5 kwa 2. Katika fainali hii makubwa yaliweza jitokeza katika uwanja wa Vancouver mbele ya hamsini elfu mashabiki baada ya Wamarekani kufunga mabao manne kwa mfululizo katika dakika kumi na tano za mwanzo wa mchezo. Carli Lloyd alifanya hila mpaka muda mfupi baada ya mechi akapatiwa taji lai mchezaji bora wa mashindano. Hata hii ni mara ya tatu katika michuano ya Kombe la dunia ya timu ya Marekani ya wanawake kutokea hila hizi.Maafisa kutoka FIFA wameshutumu uongozi wa soka duniani kwa kupingwa na umati wa watu.