Balotelli hajarejea kambini-Liverpool

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Balotelli hajarejea kambini-Liverpool

Mshambulizi wa Liverpool na Italia , Mario Balotelli hajarejea kambini Anfield kwa mazoezi ya kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Muitaliano huyo ambaye hakuwa na msimu wa kufana alipojiunga na the Reds anasemekana kuwa alifiwa.

The Reds' walirejea katika kambi ya mazoezi siku ya jumatatu baada ya likizo ndefu ya msimu wa jua.

"ningependa kuwashukuru mashabiki wangu wote''

''Familia yangu inawashukuru pia''alisema mshambulizi huyo machachari.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Balotelli alifunga bao moja pekee katika ligi ya premia

Balotelli mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kujiunga na kikosi hicho cha Liverpool kabla ya ziara ya kujipima nguvu mashariki ya mbali na Australia.

Tangu ajiunge na the Reds mshambulizi huyo wa zamani wa Manchester City hakunga'ara kama ilivyotarajiwa baada ya kununuliwa kwa kima cha pauni milioni £16m mwezi Agosti.

Alifunga mabao 4 ikiwemo moja pekee katika ligi ya premia na hakuweza kuhakikishiwa nafasi ya timu ya kwanza licha ya kutokuwepo kwa nyota kutoka Uruguay Luis Suarez.