Turan:Barca yamsajili kiungo wa Atletico

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Turan:Barca yamsajili kiungo wa Atletico

Mabingwa wa Ulaya na Uhispania, Barcelona wamemsajili kiungo cha kati wa wapinzani wao Atletico Madrid Arda Turan raia wa Uturuki.

Mabingwa hao wa ulaya wametoa kitita cha pauni milioni 24.

Kulingana na kandarasi hiyo kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 28 ataigharimu takriban pauni milioni 29 marupurupu yote yakijumuishwa.

Kinaya ni kuwa kiungo huyo wa kati hataweza kuichezea Barcelona hadi mapema mwakani kufuatia sheria na kanuni za usajili ambazo haziiruhusu klabu hicho kumsajili mchezaji mpya hadi mwakani.

Barca ilipigwa marufuku ya kuwasajili wachezaji baada ya kukiuka maadili na kanuni zilizowekwa katika usajili wa wachezaji ambao hawajahitimu miaka 18.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Barca ni mabingwa wa taji la ligi kuu ya Uhispania La Liga, Kombe la Mfalme : Copa del Rey na ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Turan aliisaidia Atletico kufunga mabao 32 mbali na yeye mwenyewe kufunga mengine 22 tangu alipotua Uhispania mwaka wa 20111 akitokea Galatasaray.

Barca vilevile imeathirika na uchaguzi unaoendelea klabuni.

Klabu hicho kiko katikati ya kampeini kali ya uchaguzi wa mwenyekiti mpya na hivyo kwa sasa kinaendeshwa na kamati maalum.

Kamati hiyo ndio inayopaswa kukamilisha uhamisho huo swala ambalo linahitaji uwiano wao wote.

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Barca iko katikati ya kampeini kali ya uchaguzi wa mwenyekiti mpya

Kulingana na kanuni za klabu hiyo ya Catalan yeyote atakayeibuka mwenyekiti mpya wa klabu hiyo aataweza kumrejesha Turan alikotoka katika kipindi cha siku 2 za utawala wake lakini kwa gharama yaasilimia 90% ya fedha zilizotumika kupata huduma zake (milioni £24.

Uchaguzi utafanyika julai tarehe 18.

Vijana wa Luis Enrique walishinda taji la ligi kuu ya Uhispania La Liga, Kombe la Mfalme : Copa del Rey na ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Awali kocha huyo alikuwa amemsajili winga wa Sevilla, Aleix Vidal kwa pauni milioni £16m .