Wimbledon:Serena na Sharapova nusu fainali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wimbledon:Serena na Sharapova kuchuana katika nusu fainali Alhamisi

Mchezaji tenis anayepigiwa upatu kushinda taji la mwaka huu la Wimbledon, Serena Williams alisajili ushindi mkubwa dhidi ya Victoria Azarenka.

Williams ambaye anapigiwa upatu kutwaa mataji yote matatu makuu ya tenis ya wanawake ama ''Grand Slam'' alimshinda mpinzani wake kwa seti tatu kwa nunge.

Muamerika huyo mwenye umri wa miaka 33, alisajili ushindi wa alama 3-6, 6-2 na kisha 6-3 mbele ya mashabiki 15,000 katika uwanja wa katikati wa Wimbledon.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Iwapo atashinda taji la wanawake , Serena huenda akatawazwa kuwa bingwa wa mataji yote manne makuu ya tenisi ya wanawake.

Kufuatia ushindi huo Serena sasa ameshinda mechi 26 mtawalia tangu mwaka wa 2014.

Williams sasa ameratibiwa kuchuana na Mrusii Maria Sharapova anayeorodheshwa wa nne bora katika nusu fainali ya mashindano hayo hapo kesho.

Iwapo atashinda taji la wanawake , Serena huenda akatawazwa kuwa bingwa wa mataji yote manne makuu ya tenisi ya wanawake.

Hii itakuwa mara ya kwanza tangu mwaka 1988 ,Steffi Graf aliposhinda mataji yote manne ya wanawake ya tenisi katika msimu mmoja.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wimbledon:Serena na Sharapova kuchuana katika nusu fainali Alhamisi

Williams na Sharapova watakuwa wakichuana kwa mara ya 20.

Serena ameshinda mechi 16 kati ya mechi hizo.

"imekuwa muda kidogo tangu tukutane japo nafahamu kuwa mekuwa akicheza vyema''.Williams aliiambia BBC Michezo.