Wachezaji wa kimataifa wawasili Azam

Image caption Nelson Lukong,mmoja kati ya wachezaji wa kimataifa watakaowasili Azam Fc.

Wachezaji watatu wa kimataifa wanatua Azam FC kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chake, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ligi kuu Tanzania Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Azam ilimaliza nafasi ya pili katka msimu wa ligi uliokwisha na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Shirikisho. Mmoja wachezaji hao ni mlinda lango Mkameruni anayekipiga nchini Congo (DRC ), Nelson Lukong, anayetegemewa kusaili usiku huu.

Mbali na Nelson Lukong leo Alhamisi saa mbili asubuhi kiungo toka nchini England Ryan Burge atawasili na Qatar Air.

Jean Mugiraneze Babtiste toka nchini Rwanda anayekipiga na APR atawasili na Rwanda Air jioni ya leo Alhamisi

Baada ya mazoezi ya wiki tatu Azam FC inasafiri leo asubuhi kuelekea mjini Tanga, Kaskazini mwa Tanzania kucheza mechi mbili za kirafiki. Itacheza na African sports wana kimanumanu siku ya Jumamosi na Jumapili itakwaana na Coastal Union Mechi zote mbili zitachezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani majira ya jioni.

Timu itarejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu.