Mo Farah kurejea michezoni

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mo Farah

Bingwa mara mbili wa mashindano ya Olympic Mo Farah ametamka bayana kuwa anarejea ulingoni kwa mara ya kwanza baada ya kuwepo kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kusisimua misuli dhidi ya kocha wake Alberto Salazar.

Farah anayedai kuwa yupo safi kwa asilimia mia na hana doa, atapambana na mchezaje mwenzake Andy Vernon kwenye michuano ya mita elfu tano ya Diamond huko mjini Lausanne nchini Switzerland.

Mbio hizo za mita elfu tano ni za kwanza kwa Mo Farah katika msimu huu lakin pia ni mara kwanza kwa yeye kukimbia katika kipindi cha wiki sita.