Kocha;Taifa Stars awashukuru watanzania

Image caption Kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface ,aliyeinua mkono.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa amewashukuru Watanzania wote waliowapa sapoti katika mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda uliochezwa mwishoni mwa wiki jijini Kampala.

Mkwasa amesema kujitolea kwa wachezaji wa Taifa Stars (uzalendo) katika mchezo huo kulipelekea kuwapa wakati mgumu wenyeji, huku watanzania waliojitokeza kuja kushuhudia mchezo huo wakiwashangilia muda wote wa mchezo. Uganda (The Canes) ilitoka sare ya 1-1 katika mchezo huo na kusonga mbele kwa jumla ya magoli 4-1.

“Kiukweli japo timu haikuweza kupata matokezo mazuri sana, lakini tunamshukuru Mungu ndani ya wiki moja ya maandalizi, tumeweza kuwapa maelekezo vijana na kuyafanyia kazi, japo wengine walikua wakicheza kwa mara ya kwanza timu ya Taifa walicheza vizuri, kijumla wote kwa pamoja walifanya vizuri sana katika mchezo dhidi ya Uganda” alisema Mkwasa.