All Afrika Games CAF yataja makundi

Image caption Twiga stars mazoezini

Upangaji wa makundi wa soka ya wanawake ya Michezo ya Afrika (All Africa Games) itakayofanyika nchini Congo Brazzaville kuanzia Septemba 4-19 umefanywa na Shirikisho la soka barani Afrika, CAF na timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imepangwa Kundi A pamoja na wenyeji Kongo, Nigeria na Ivory Coast.

Upangaji wa makundi hayo umefanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri.

Kundi B lina timu za Cameroon, Afrika Kusini, Ghana na Misri. Upande wa wanaume, Kundi A lina timu za Kongo, Sudan, Zimbabwe na Burkina Faso, wakati Kundi B kuna Ghana, Senegal, Misri na Nigeria.