Tyson Gay:Sitaki kuitwa muongo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Tyson Gay

Mwanariadha wa mbio fupi raia wa Marekani Tyson Gay ametaka kutoitwa mtumiaji wa dawa za kusisimua misuli.

Gay mwenye umri wa miaka 32 ,alihuduamia marufuku ya mwaka mmoja baada ya kupatikana alitumia dawa hizo mwaka 2013.

Anatarajiwa kushindana na Justin Gatlin na Asafa Powel wote wakiwa walihudumia marufuku walipotumia dawa za kusisimua misuli.

Mashindano hayo yatafanyika katika mkusanyiko wa mbio za Diamond League mjini Lausanne siku ya alhamisi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tyson Gay

''Wakati unapolihusisha jina la mtu na uovu ,inabadili fikra za watu na kuanza kuamini kwamba ulijaribu kufanya uovu na ukafanikiwa'',alisema Gay.

''Lakini hiyo haikuwa dhamira.Iwapo ningefanya uamuzi wa kufanya kitu kwa makusudi ili kuathiri riadha, nisingerudi.