Nijel Amos amshinda tena Rudisha

Image caption Nijel Amos

Bingwa wa rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 Dunia mkenya David Rudisha ameshindwa tena kwa mara nyengine katika mbio hizo na Bingwa katika mbio hizo Nijel Amos wa Botswana.

Rudisha tayari alikuwa ameongoza mbio hizo akiwa mbele na ilikuwa imesalia mita 300 kufika katika utepe,wakati Nijel Amos alipotoka nyuma na kumshinda.Rudisha

Image caption David lekuta Rudisha

wakati huohuo mwanariadha wa Marekani Justin Gatlin aliweka mda bora wa pili mwaka 2015 baada ya kumshinda Asafa Powel na Tyson Gay katika mbio za mita 100 katika mbio za Diamond League mjini Lausanne.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye amehudumia mara mbili marufuku ya kutumia dawa za kusisimua misuli alikimbia mda wa sekunde 9.75 kabla ya mashindano ya mwezi ujao ya dunia.

Powell na Gay wote wamekimbia mda wa sekunde 9.92 huku Usain Bolt akiwa bado anauguza jeraha,ijapokuwa ana mpango wa kutetea taji lake katika mbio za Olimpiki mjini Beijing.

Image caption Rudisha

Tyson Gay na Jamaica Powell pia walihudumia marufuku ya kutumia dawa za kusisimua misuli.

Gay mwenye umri wa miaka 32 alihudumia marufuku ya mwaka mmoja baada ya kupatikana ametumia dawa hizo aina ya anabolic steroid mwaka 2013,huku Powell akihudumia marufuku ya miezi sita baada ya kupatikana ametumia dawa hizo mwaka 2013.