Tenis:Serena ni bingwa wa Wimbledon

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Serena Williams 6-4,6-4 Garbine Muguruza

Serena Williams ndiye mshindi wa tuzo la Wimbledon la wanawake mwaka huu.

Image caption Serena Williams ndiye mshindi wa tuzo la Wimbledon la wanawake mwaka huu.

Serena alitawazwa kuwa bingwa mwaka huu baada ya kumlaza mpinzani wake Garbine Muguruza seti mbili kwa nunge katika fainali ya mchuano huo huko Uingereza.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Williams mwenye umri wa miaka 33 ameandikisha rekodi ya kuwa mshindi wa matuzo hayo mwenye umri mkubwa zaidi.

Raia huyo wa Marekani aliandikisha rekodi ya kuwa mshindi wa kwanza wa mataji manne ya tenis ya wanake kwa wakati mmoja.

Image caption Serena Williams alimshinda mpinzani wake seti 2-0

Aidha Williams mwenye umri wa miaka 33 ameandikisha rekodi ya kuwa mshindi wa matuzo hayo mwenye umri mkubwa zaidi.

Serena aliandikisha alama 6-4 katika seti ya kwanza na kisha alama sawa na hizo katika seti ya pili.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kufuatia ushindi huo Williams alijinyakulia taji lake la 21 na la tatu katika msimu huu wa 2015.

Kufuatia ushindi huo Williams alijinyakulia taji lake la 21 na la tatu katika msimu huu wa 2015.

Image caption Serena sasa anashikilia mataji 4 ya tennis ya wanawake

Kwa upande wake Muguruza, mwenye umri wa miaka 21 na aliyeorodheshwa katika nafasi ya 20 alijikakamua na kustahimili wimbi la mashambulizi makali kutoka kwa bingwa huyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Williams alijinyakulia taji lake la 21 na la tatu katika msimu huu wa 2015.

Raia huyo wa Uhispania alistahimili kishindo hicho kwa zaidi ya saa moja na dakika 23 kabla ya kusalimu amri.

Mashindano yajayo yatakuwa nchini Marekani.