Miaka 2 nje kwa Chennai na Rajasthan Royals

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Miaka 2 nje kwa Chennai na Rajasthan Royals

Vilabu viwili vikubwa vinavyoshiriki ligi ya kriketi nchini India vimepigwa marufuku ya miaka 2 baada ya kupatikana na hatia ya kupanga mechi

Maafisa kutoka Chennai Super Kings na Rajasthan Royals walipatikana na hatia kwa kushirikisha kamari katika michezo hiyo.

Jopo lililoteuliwa na mahakama ya juu zaidi nchini India kuchunguza tuhuma za rushwa katika mchezo wa kriketi, limependekeza kwamba vilabu hivyo viwili vya juu katika mashindano ya premia visitishwe kucheza kwa miaka miwili.

Maafisa wakuu wa klabu hizo wanadaiwa kupanga mechi za ligi hiyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raj Kundrana na Gurunath Meiyappan wa Super Kings wamepigwa marufuku maisha

Raj Kundrana na Gurunath Meiyappan wa Super Kings walipatikana na hatia hiyo ya jopo hilo la maafisa na wakapigwa marufuku ya kushiriki shughuli zozote za Kriketi.

Tangu kuzinduliwa kwake miaka 7 iliyopita, IPL imekuwa ligi tajiri zaidi ya kriketi.

Wachezaji nyota wa India na wale wa kimataifa hushiriki ligi hiyo kila mwaka.

Haki miliki ya picha PTI
Image caption Rajasthan Royals walishinda taji la kwanza 2008

Chennai Super Kings inaongozwa na nahodha wa India MS Dhoni,huku Royals ikiongozwa na nahodha Steve Smith kutoka Australia .

Chennai imeshiriki katika fainali nne za mashindano hayo na kutwaa ubingwa katika mwaka wa 2010 na 2011.

The Royals walitwaa taji la ufunguzi mwaka wa 2008.