Novat Djokovic atwaa taji

Image caption Novak Djokovic ashinda mashindano ya Wimbledon

Mserbia Novak Djokovic ameshinda taji la Wimbledon baada ya kumfunga mpinzani wake wa mara zote Roger Federer.

Djokovic ametetea ubingwa wake mara mbili mfululizo mara zote akimpiga mpinzani wake Federer. Roger Federer ni mshindi mara saba wa Wimbledon na wawili hawa wamewahi kukutana mara 40 na kila mmoja kamfunga mwenzake mara 20.

Kama si kipigo hicho kwa Federer alikuwa na matumaini ya kuwa mwanaume wa kwanza kushinda Wimbledon mara nane.

Novak mwenye miaka 28, alishinda kwa 7-6 (7-1) 6-7 (10-12) 6-4 6-3