Sunday Oliseh kuinoa Super Eagles

Image caption Sunday Oliseh awa kocha wa Super Eagles ya Nigeria

Timu ya Taifa ya Nigeria Super Eagles imempa kibarua cha ukocha kiungo na nahodha wake wa zamani Sunday Oliseh mwenye miaka 40 hivi sasa.

Oliseh anachukua mikoba ya Stephen Okechukwu Keshi ambaye alitimuliwa mwanzoni mwa mwezi huu.

Akizungumza na BBC Oliseh amejigamba kwa kusema, "Tuna vipaji vya kuleta mabadiliko, kurejesha heshima ambayo tuliwahi kuwa nayo. Kwa mpira wa Afrika hii ni kazi kubwa lakini Kwa kushirikiana na kila mtu Super Eagles watapaa tena"

Hata hivyo katika kibarua chake hicho cha ukocha Oliseh atasaidiwa na mbeligiji Jean Francois Losciuto wakati huu kikosi hicho kikiwa kunajkupambana na Tanzania mapema mwezi wa Septemba mwaka huu katika michuano ya kufuzu kombe la mataifa afrika la mwaka 2017.