Arsenal yasaka sahihi ya Benzema

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Karim Benzema asakwa na Arsenal

Arsenal wameripotiwa kujiandaa 'kuvunja benki' kwa lengo la kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema.

The Gunners kwa mda mrefu wamekuwa wakihusishwa na uhaimisho wa Benzema na sasa wako tayari kukamilisha lengo lao.

Kulingana na gazeti la The Sun ,wakuu wa Arsenal wanatarajiwa kutoa kitita cha dola milioni 40 ili kumtia mkobani raia huyo wa Ufaransa ambaye wanaamini anataka kutoka Uhispania.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Benzema

Mkufunzi mpya wa Real Madrid Rafa Benitez alifichua mpango wake wa kumchezesha mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kama mshambuliaji mkuu.

Mpango huo tayari unamsukuma mbali Benzema ambaye hayuko tayari kucheza kama mchezaji wa ziada.

Gazeti la The sun lina ripoti kwamba kocha wa Arsenal Arsene Wenger amewasiliana na Real kuhusu uhamisho huo na mazungumzo yanaendelea.