Manchester United yailaza Club America

Haki miliki ya picha empics
Image caption manchester United

Morgan Schneiderlin aliifungia Manchester United bao moja dakika tano baada ya kuingia huku timu hiyo ikiishinda Klabu ya Mexico Club America 1-0 huko Seattle.

Wachezaji wapya wa Manchester United akiwemo Schneiderlin,Memphis Depay na Matteo Renzi walishiriki katika mechi hiyo.

Bastian Schweinsteiger alikuwa mmoja ya wachezaji 11walioingia katika kipindi cha pili.

Bao la Schneiderlin lilikuwa muhimu sana katika kuipatia ushindi Manchester United,baada ya kiungo huyo aliyesajiliwa kwa pauni milioni 25 kutoka Southampton kupata krosi safi ya Juan Mata.