Manchester City yamsajili Fabian Delph

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Aliyekuwa nahodha wa Aston Villa Fabian Delph

Nahodha wa kilabu ya Aston Villa Fabian Delph amekuwa mchezaji wa hivi karibuni kujiunga na kilabu ya Mancity siku chache tu baada ya kusema kuwa atasalia katika uwanja wa Villa Park.

Uhamisho wa mchezaji huyo wa Uingereza kuelekea Mancity nusra ugonge mwamba baada ya mchezaji huyo kusema kuwa atasalia Aston Villa.

City walikubali kumnunua mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 8 huku mchezaji huyo akiweka sahihi ya kandarasi ya miaka minne na nusu.

''Akiwa na umri wa miaka 25,Delph ana miaka ya matumaini mbele yake'', alisema mkufunzi wa City Manuel Pellegrini.