Fillipe Luis kuondoka Chelsea

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Filipe Luis

Mlizi wa kushoto wa Chelsea Filipe Luis anakaribia kuihama klabu hiyo baada ya kuichezea kwa mwaka mmoja, hii ni kwa mujibu wa kocha mkuu wa timu hiyo Jose Mourinho.

Mchezaji huyo raia wa Brazil amechezea mara 26 tangu aliposajiliwa na Chelsea akitokea Atletico Madrid kwa kitita cha paundi milioni 15.8 wakati wa msimu wa joto. Hata vilabu hivyo viwili vimekubaliana mchezaji huyo arejee kwenye klabu yake ya zamani.

Mourinho amesema" Kwa wakati huu tunahitaji beki wa kushoto kwa sababu nafikiri tutamuuza Fillipe Luis leo au kesho.

Chelsea inadaiwa kuwa ina mpango wa kumnunua beki wa kushoto kutoka Augsburg, Abdul Baba Rahman.