Benteke ahamia rasmi Liverpool

Image caption Christian Benteke

Timu ya livepool imekamilisha kumsajili rasmi mshambuliaji mwenye asili ya Jamuhuri ya Kidemokrasia wa kongo Christian Benteke kutoka Aston Villa kwa kitita paundi milion 32.5.

Benteke alikubali mkataba wa muda mrefu na kuwa mchezaji wa pili kununuliwa kwa gharama kubwa huko England.

Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji ameifunga magoli 49 katika mechi 101 alizocheza kwenye timu yake ya zamani ya Aston Villa.