Dzeko kuondoka Man City

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Edin Dzeko

Kocha Mkuu wa Manchester City Manuel Pellegrini amekubali kuwa mshambuliaji wake Edin Dzeko anaweza kuondoka kwenye klabu hiyo.

Dzeko mwenye miaka 19 yupo pamoja na kikosi cha Man City katika safari ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi huko Australia na hakucheza wakati timu hiyo ilipocheza na AC Roma ya Italia siku ya jumanne.

Kuna taarifa Dzeko huenda anaweza kuhamia kuchezea moja ya vilabu huko nchini Italia.