Keshi kudai shirikisho Euro milioni 3.2

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Steven Keshi

Kocha wa zamani nchini Nigeria,Stephen Keshi anaidai shirikisho la soka nchini humo Euro milioni 3.2 kwa kufukuzwa kazi kabla ya mkataba wake kuisha.

Keshi ambaye alifukuzwa kazi mwanzoni mwa July na nafasi yake kuchukuliwa na Sunday Oliseh.Aliiandikia shirikisho la soka nchini Nigeria NFF kupitia wakili wake kwa kutoa madai ya kuchafuliwa kwa kashfa na habari zisizo na ukweli. Hata hivyo msemaji wa shirikisho hilo anasema NFF haiko kwenye nafasi ya kumlipa hivyo ana uhakika shirikisho halitaweza kulipa fedha hizo kwa kushurutishwa na Keshi.

BBC imebaini kuwa Keshi anajaribu kulinda heshima yake na wasifu katika duru za soka baada NFF kamati ya nidhamu kumpa madai mbalimbali dhidi yake. Keshi bado hajapeleka kesi yake mahakamani akiwa ana matumaini kuwa suala lake linaweza kutatuliwa ndani ya shirikisho. Kocha wa zamani wa Togo na Mali ambaye alikua kocha wa pili wa zamani wa Nigeria a katika kipindi cha miaka mitano aliishitaki NFF katika hatua za kisheria mnamo oktoba 2011.kwa kosa la kumfukuza msaidizi wake Samson Siasi lakini baadaye aliondoka kesi hiyo na alisema alitaka kusonga mbele.

Keshi , kocha wa zamani wa timu ya taifa , aliiongoza timu yake katika mashindano ya mwaka 2013 ya Kombe la Mataifa ya Afrika Kusini na pia aliongoza Super Eagles katika Duru ya 16 katika Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Mkataba wake haukuwa mpya baada ya Kombe la Dunia lakini baadae alipewa wa mechi kwa mechi , ambao ulikua umalizika mwezi Novemba baada ya kushindwa timu hiyo kufikia fainali za Kombe la Mataifa mwaka 2015.