Robo fainali Kagame kuanza leo

Image caption APR,Al Khartoum,Gormahia na Malakai kujitupa uwanjani leo

Hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Cecafa Kagame Cup itachezwa leo kwa michezo miwili kupigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo wa kwanza utakua kati ya Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR ya Rwanda itacheza na Al Khartoum kutoka nchini Sudan,

Katika mchezo wa pili Gor Mahia mabingwa mara tano wa michuano ya Kagame watashuka dimbani kucheza na Malakia kutoka Sudan Kusini,

Robo fainali zitaendela siku ya jumatano, ambapo michezo miwili itachezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika hatua hiyo ya robo fainali endapo timu zitacheza kwa dakika 90 na mchezo kumalizika kwa sare, hatua itakayofuata ni kumpata mshindi kwa mikwaju ya penati.