Mshambuliaji wa Congo yuko hali mahututi

Image caption Ndey

Mshambuliaji wa timu ya Congo Rudy Guelord Bhebey Ndey yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuanguka na kichwa wakati wa mechi.

Mchezaji huyo ambaye ni nahodha wa kilabu ya AC Leopards aliumia katika dakika ya 17 wakati wa mechi ya kundi ba kati ya timu yake na ile ya Zamalek kutoka Misri siku ya jumamosi.

Alipelekwa katika hospitali maalum ya jeshi la hewani mjini cairo na kuwasili akiwa katika hali mbaya.

Image caption Ndey baada ya kuanguka uwanjani

Siku ya jumanne daktari Salah Abdlekhaleq alisema kuwa mchezaji huyo alikuwa anaendelea vyema lakini ilikuwa mapema mno kusema kuwa atacheza tena.

''Alikuwa na majeraha mabaya katika uti wake wa mgongo kati ya mfupa wa tano na wa sita ambalo ni pigo kubwa kwa uti huo,alikuwa na matatizo ya kupumua mbali na kuvuja damu kutoka kwa ubongo'', alisema daktari.