Mourinho:Benitez aliiharibu Inter Millan

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mourinho

Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho amemshtumu kocha wa Real Madrid Rafael Benitez kwa kuiharibu timu bora Ulaya baada ya Benitez kumrithi katika kilabu ya Inter Milan mwaka 2010.

Mkufunzi huyo wa Chelsea alizungumza baada ya mkewe Benitez kufanya mzaha kwamba alikuwa anasafisha tena 'uharibifu' ulioachwa na Mourinho katika kilabu ya Real Madrid.

Pamoja na Real Madrid ,Benitez pia aliifunza Chelsea ijapokuwa hakumrithi moja kwa moja Mourinho katika vilabu vyote.

''Huyu mwanamke nadhani amechanganyikiwa'',Mourinho alisema baada ya timu yake kuishinda Barcelona katika kombe la ubingwa wa kimataifa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Benitez

''Mumewe alienda Chelsea kumrithi Roberto Di Matteo na alienda Real Madrid kumrithi Carlo Ancelotti''.

"Kilabu ya pekee ambapo alinirithi ni ile ya Inter Milan ambapo baada ya miezi sita alikuwa ameiharibu timu iliokuwa bora Ulaya wakati huo''.