Miguel Herrera afutwa kazi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Miguel Herrera kocha wa Mexico aliyefukuzwa kazi

Kocha kutoka Mexico, Miguel Herrera amefukuzwa kazi baada ya kumshambulia mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha luninga.

Hatua hii ya kufukuzwa kazi kwa kocha huyo kunakuja ikiwa ni mbili tu baada ya kuongoza kikosi hicho kwenye kombe la saba la medali ya dhahabu nchini Marekani.

Miguel Herrera mwenye umri wa miaka 47 amekuwa akiiongoza timu hiyo ya Mexico kwa miaka16 hadi sasa. katika utetezi wake Herrera amesema kuwa alifanyiwa fujo ndo maana akafikia hatua hiyo.