Arsenal kupambana na Chelsea

Haki miliki ya picha AP
Image caption Chelsea na Arsenal

Ligi kuu ya Uingereza inaanza tena siku ya jumapili wakati ambapo mabingwa wa ligi hiyo Chelsea wanakutana na washindi wa kombe la FA Arsenal katika kombe la Charity Shield itakayogaragazwa katika uwanja wa Wembley.

Mechi hiyo inajiri siku 64 baada ya kumaliza ligi hiyo na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika fainali ya FA.

Pende zote mbili hazijafanya usajili mkubwa katika msimu huu ijapokuwa kipa Petr Cech ataanzishwa dhidi ya timu yake ya zamani Chelsea.

Haki miliki ya picha Arsenal.com
Image caption Petr Cech

Chelsea vilevile inaweza kumuanzisha mchezaji wao mpya Radamel Falcao.

Falcao mwenye umri wa miaka 29 alihudumu katika kilabu ya Manchester United msimu uliopita lakini hakuweza kutamba kwani aliweza kufunga mabao 4 katika mechi 29 alizocheza pekee.

Siku ya jumapili itazikutanisha timu hizo mbili huku mkufunzi wa Arsenal akitarajia kuishinda timu inayofunzwa na Mourinho kwa mara ya kwanza kati ya mechi 13 walizocheza huku wakufunzi hao wawili tayari wakitofautiana.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wenger na Mourinho

Mourinho alisema kwamba Arsenal imetumia fedha nyingi msimu huu ikilinganishwa na Chelsea katika kipindi cha miaka kadhaa iliopita ,huku Wenger akijibu kwamba hasikizi kile watu wanachosema ama kufikiri.