Azam bingwa Cecafa

Image caption Azam ilicheza mchezo wa Fainali kombe la CEcafa

Timu ya soka ya Azam Fc ya Tanzania imeutwaa ubingwa kwa kombe la Cecafa kagame Cup kwa mwaka 2015.

baada ya kuichapa timu ya Gor Mahia ya Kenya kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainalia uliofanyika katika uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam Tanzania.

Mabao ya Azam maarufu kama wanalambalamba yalifugwa na washambuliaji wake John Bocco na Kipre Tchetche aliyepiga mpira wa adhabu nakuzama moja kwa moja nyavuni.

Wanalamba lamba hao wametwaa uchampion huu wa kwanza bila ya nyavu zake kutikiswa.

Katika mchezo wa awali KCCA ya Uganda iliichapa Al Khartoum 2-1 na kutwaa nafasi ya Mshindi wa 3 wa Kagame Cup.

Bao za KCCA zilifungwa na Michael Birungi na Muzamir Mutyaba na lile la Al Khartoum kuingizwa na Ousmaila Baba.

Azam FC kwa kuwa Mabingwa wa Kagame Cup wamezoa Kombe pamoja na kitita cha Dola 30,000 huku Gor Mahia wakipata Dola 20,000 na KCCA Dola 10,000