David Rudisha ashindwa nyumbani

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rudisha

Bingwa wa mbio za Olimpiki anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 David Rudisha alishindwa kwa mara ya kwanza nyumbani Kenya.

Rudisha mwenye umri wa miaka 26,alichukua nafasi ya pili nyuma ya mwanariadha Ferguson Rotich mwenye umri wa miaka 25 jijini Nairobi.

Hatahivyo Rudisha atashiriki katika mashindano hayo yatakayofanyika Beijing baadaye mwezi huu.

''Nimeshtushwa na kushindwa kwangu lakini ninafurahi niko katika timu ya taifa'', alisema Rudisha ambaye alidai kwamba bado haijamarika vilivyo.

Rudisha alishinda ubingwa wa mita 800 mjini Daegu mwaka 2011 lakini akakosa riadha za ubingwa mjini Moscow kupitia jeraha alilopata.

''Bado sijafanya zoezi lakuimarisha kasi yangu,ijapokuwa niko aslimia 90 tayari.

Kwa sasa nimesalia na wiki tatu kuimarisha kasi aliongezea.