Di Maria njiani kuelekea PSG

Haki miliki ya picha AP
Image caption Winga wa Manchester United Angel Di Maria

Winga wa klabu ya soka ya Manchester United Angel Di Maria anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya ndani ya saa 24 zijazo ili kuweza kuijiunga na miamba wa soka Ufaransa Paris St-Germain.

De Maria alivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza baada ya kusajiliwa na Manchester United kwa kiasi cha pauni milioni 59.7 anatarajiwa kukutana na maofisa wa PSG huko Doha siku ya jumatatu ili kukamilisha uhamisho huo.

Inaaminika kuwa nyota huyo wa Argentina mwenye miaka 27 atauzwa kwa kiasi cha pauni millioni 44.5.

Di maria hakuungana na wachezaji wenzake wa Man United waliokua katika ziara ya kujiandaa na msimu mpya huko Marekani baada ya kutoka kwenye michuano ya Copa America.

Winga huyu alianza kukitumikia kikosi cha mashetani wekundu vizuri mwanzoni mwa msimu uliopita kabla ya kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza.

Huku akianza mchezo mmoja tu tangu United walipopoteza mchezo dhidi ya Arsenal katika mchezo wa kombe la Fa uliofanyika mwezi Machi.