Wenger:Ushindi dhidi ya Chelsea ni muhimu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfungaji wa bao la pekee dhidi ya Chelsea Oxlade-Chamberlain

Mkufunzi wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger anaamini kwamba wachezaji wake walipita kikwazo kikuu kwa kuwashinda Chelsea siku ya jumapili katika kombe la Charity Shield.

Arsenal ilikuwa haijaishinda Chelsea chini ya ukufunzi wa Mourinho katika mechi 13 walizocheza kati yao.

Lakini bao la mchezaji Oxlade-Chamberlain dhidi ya mabingwa hao wa ligi ya Uingereza liliwapatia ushindi Arsenal katika uwanja wa Wembley.

''Ilikuwa muhimu kwa timu yetu kupita kikwazo hiki kikubwa cha kifikra'', alisema Wenger.