Kenya yakanusha kushiriki udanganyifu

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kenya yakanusha kushiriki udanganyifu na njama ya kuficha matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini

Shirikisho la riadha nchini Kenya limekanusha kuhusika na udanganyifu na njama ya kuficha matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini miongoni mwa wanariadha wake.

Hii inafwatia ripoti iliyochapishwa na vyombo vya habari nchini Uingereza na kupeperushwa na runing moja ya Ujerumani mwishoni mwa juma.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari,Shirikisho hilo la riadha la Kenya linasema kuwa hii ni njama ya wapinzani wa Kenya ambao wanfahamu fika kuwa upinzani wao mkubwa unatokea hapa (Kenya).

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bingwa wa mbio za Boston Marathon Rita Jeptoo anatumikia marufuku ya miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madawa haramu ya kuongeza nguvu mwilini

''hii sio sadfa kuwa ripoti hii imetokea wakati ambao Kenya ilikuwa ikichagua kikosi kitakachoiwakilisha katika mashindano ya dunia katika uwanja wa Kasarani mjini Nairobi, tunashuku kuwa hii ni njama ya kuwavunja moyo wanariadha wetu na kufanya washindi wetu wadhaniwe kuwa wanatumia madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini'' ilisema taarifa hiyo.

''Ripoti hiyo inatoa taarifa za uongo tu''

'Chanzo cha ripoti hiyo ni takwimu na utafiti ulioibiwa, itakuwaje habari hizo zisadikike ?'

''Shirikisho la riadha la Kenya limehakikisha kuwa mlango wake uko wazi na ikiwa kuna mtu yeyote mwenye ushahidi wa kutosha basi, anaweza jitokeza ili uchunguzi ufanyike na kisha ukweli ubainike'' Ripoti hiyo inasema.

Haki miliki ya picha
Image caption A. K inasema kuwa hizi ni njama za kutibua maandalizi ya timu ya Kenya

''Miaka mitatu iliyopita runinga hiyo hiyo ya Ujerumani ilipeperusha ripoti sawa na hii na mwandishi wake Hajo Seppelt, alikusudia kuwatia baridi wanariadha wakenya walipokuwa wakielekea kwenye mashindano ya kimataifa,hilo halikufaulu wala haitafaulu mwaka huu.''

''Timu yetu ya wanariadha itaendelea na mazoezi yake ya kujiandaa kupeperusha bendera ya Kenya katika mashindano ya riadha ya dunia huko Beijing Uchina.''

Mwandishi huyo hajajitokeza kuiuliza shirikisho la riadha la Kenya maswali yeyote,itakuwaje basi anapeperusha matangazo na madai kama hayo bila ya kutupa fursa ya kujibu madai dhidi yetu?'' Taarifa hiyo inauliza.

Tumewaashauri mawakili wetu kuitizama ripoti hiyo kwa kina kwa nia ya kuwafungulia mashtaka kwa kuichafulia jina shirikisho na maafisa wake wa sasa na wale waliokuwepo awali.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanariadha wakenya wametawala mbio za masafa wastani na masafa marefu ya Marathon

Uchunguzi ulioendeshwa na gazeti la Uingereza la Sunday Times na kituo cha habari cha Ujerumani cha ARD, baada ya taarifa zilizovuja za maelfu ya matokeo ya uchunguzi wa damu kutoka kwa shirikisho hilo kuonesha kuwa mashrikisho ya riadha hayajakuwa yakiwajibika ipasavyo na mengine haswa yakificha ukweli.

Shirikisho la riadha duniani IAAF imetetea jitihada zake za kupambana na matumizi ya madawa ya kusisimua misuli kwa kuongeza idadi na ubora wa vifaa vinavyotumika kupima matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini.

BBC inaendelea kuwatafuta viongozi wa shirikisho waliotajwa na itakuletea habari pindi tutakapozungumza nao.