Mulumbu kuukosa mwanzo wa msimu England

Image caption Kiungo wa Norwich City, Youssouf Mulumbu

Kiungo mpya wa timu ya Norwich City Youssouf Mulumbu ataukosa mwanzo wa msimu mpya wa ligi kuu ya England.

Kiungo huyu aliyejiunga na Norwich katika majira ya kiangazi amevunjika mfupa wa kidole gumba cha mguuu hivyo atakua nje kwa wiki kadhaa kwa ajili ya matibabu

Mulumbu ambae ni raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliumia katika mchezo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi utakaoanza jumamosi ijayo.

Kocha wa Norwich Alex Neil amesema itamchukua wiki kadhaa kwa mchezji huyo kupona na kuweza kuwa fiti kwa mikikimikiki ya ligi kuu ya England.