Rafael kujiunga na Lyon

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Beki wa kulia wa Manchester United, Rafael da Silva

Klabu ya Lyon ya Ufaransa imemsajili beki wa kulia wa Manchester United Rafael da Silva kwa mkataba wa miaka minne na kwa kitita ambacho hakikutajwa.

Rafael mwenye miaka 25 alijiunga na Manchester United akiwa na pacha wake Fabio kutoka Fluminense mwaka 2008.

Katika msimu uliopita beki huyu alianza katika michezo sita tu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mara kwa mara.

Kupitia mtandao wake wa twitter Rafael aliandika "nataka kuwashukuru mashabiki kwa mapenzi kwa miaka minane niliyokuepo hapo''

Rafael amecheza jumla ya michezo 170 na akifunga mabao 5 pacha wake Fabio alijiunga na Cardiff City katika msimu wa 2014.