Di maria afurahia kujiunga na PSG

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Winga wa Timu ya taifa,Argentina Angel Di Maria

Winga wa timu ya taifa ya Argentina Angel Di maria amefurahishwa na uhamisho wake toka Manchester United na kujiunga na matajiri wa Psg.

Nyota huyu mwenye umri wa miaka 27 alifanyiwa vipimo vya afya huko Qatar na kukamilisha uhamisho wake uliogharimu kiasi cha pauni milioni 44.3.

Baada ya uhamisho huo kukamilika Di Maria alisema ana furaha kujiunga na Paris St –German .Lakini vilabu vya Manchester United na Psg havijatangaza rasmi kukamilika kwa uhamisho huo .

Di Maria alijiunga na mashetani wekundu msimu uliopita akitokea Real Madrid ambapo alicheza michezo 32 na kufunga mabao 4.