James Guy abeba medali ya dhahabu

Image caption Mshindi wa medali ya dhahabu michuano ya dunia ya kuogelea

Muingereza James Guy ameshinda medali ya dhahabu katika michuano ya kuogelea ya dunia inayofanyika Urusi.

Guy alishinda katika mbio za mita 200 ya mitindo huru na kumzidi mshindi wa medali ya shaba ya michezo ya Olimpiki Sun Yang wa China aliyeshika nafasi ya pili.

Paul Biedermann ambae anashikilia rekodi ya dunia alishika nafasi ya tatu pamoja na Ryan Lochte

Mpaka sasa Australia na Uingereza wanaongoza kwa medali wakiwa na medali 5, wakifuatiwa Marekani yenye medali 4 huku China na Ufaransa wakiwa na medali tatu kila mmoja.