Mayweather kupanda ulingoni septemba

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Floyd Mayweather

Bondia Floyd Maywether atapanda tena ulingoni mwezi Septemba 12 mwaka huu kuzipiga na Andre Berto.

Floyd atajaribu kuifikia rekodi ya bondia Rocky Marciano, ya kupigana mapambano 49 pasipo kupoteza.Berto ameshinda mapambano 30 huku akipoteza mapambano matatu.

Bondia mwingereza Amir Khan alikua na matumaini ya kuzipiga na Mayweather, baada ya kumpiga Chris Algieri, mwezi Juni.

Mayweather alieleza baada ya pambano lake na Manny Pacquiao kuwa atacheza pambano moja tu la mwisho kabla ya kustaafu mchezo wa masubwi.