Twiga Stars kuingia kambini leo

Image caption Timu ya soka ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuingia kambini leo kisiwani Zanzibar.

Kambi hii ni ya kujiandaa na fainali za michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofayika mwezi Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzavile.

Kikosi hicho cha wachezaji 25 chini ya Kocha Mkuu Rogasian Kaijage, tayari kimeanza mazoezi kujiandaa na michuano hiyo ambapo Tanzania ilikata tiketi ya kushiriki fainali hizo baada ya kuiondoa Zambia kwa jumla ya mabao 6-5.

Fainali za Michezo ya Afrika itaanza kutimua vumbi Septemba 4 mpaka Septemba 17, huku Twiga Stars ikiwa imepangwa kundi A na wenyeji Congo Brazaville , Nigeria pamoja na Ivory Coast.