Michuano ya dunia Mpira wa pete kuanza

Image caption Michuano ya mpira wa pete kuanza leo

Michuano ya kumi na nne ya Kombe la dunia la mchezo wa pete itaanza kutimua vumbi leo katika jiji la Sydney nchini Australia.

Jumla ya michezo sitini na minne itacheza katika siku kumi za michuano hiyo ambapo timu kumi na sita zitachuana kuwania ubingwa wa dunia.

Viwanja viwili vya Allphones na City Olympic Park ndio vitatumika katika michuano hii.

Katika kundi A kuna wenyeji Australia, New Zealand , Barbados,Trinidad & Tobago.

Kundi B lina timu za England,Jamaica,Scotland na Samoa.

Kundi C Afrika Kusini,Malawi,Sri Lanka, Singapore.

Kundi D kuna timu za Fiji, Wales , Zambia, Uganda.